Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma ndani safari ya Morocco

Beki Shabani Djuma

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Yanga inatarajia kuelekea Morocco Jumapili lakini ikimtangaza golikipa, Erick Johora Mtanzania aliyekuwa akiichezea klabu ya Aigle Noir ya Burundi kuwa sasa ni mali yao.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema Djuma ni mchezaji wao na anakanusha propaganda za kuonyesha hawajamsajili mchezaji huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

"Naona propaganda nyingi zinaendelea. Huyu ndiye mchezaji wa kwanza sisi kumsajili. Labda tu wengi wanaona si kweli kwa sababu hatujamtambulisha".

Tumeshindwa kufanya hivyo kwa sababu hajafika Dar es Salaam. Ni mchezaji ambaye atafika nchini ifikapo terehe 14 (Jumamosi) na ataungana na kikosi tayari kwa safari ya kwenda Morocco," alisema Bumbuli.

Kiongozi huyo alisema baada ya kuondoka kwa nyota wao, Tuisila Kisinda sasa nafasi za wachezaji wa kigeni zimebaki mbili, na wachezaji watakaochukua nafasi hizo watatangazwa wakati wowote.

Aliongeza kikosi chao kinatarajia kuweka kambi ya siku 10 huko Morocco na msafara wao utakuwa na watu 44. Ofisa Habari huyo pia aliongeza kilele cha Wiki ya Mwananchi itakuwa ni Agosti 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Naye Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, alisema mchakato wa usajili wa timu yao unakwenda vizuri na anaamini utawapa matokeo chanya.

“Tuliahidi kusajili wachezaji ambao wataleta ushindani ndani ya timu yetu kwa kuwa mikakati tuliyonayo kwa sasa ni kuchukua ubingwa kwa msimu ujao pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa," Msolla alisema.

Imeandikwa Adam Fungamwango na Shufaa Lyimo

Chanzo: ippmedia.com