Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma Shabani kumchomoa mmoa Azam FC

Djuma Shabaniii.jpeg Djuma Shabani kumchomoa mmoa Azam FC

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Azam FC juzi ilipata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Arta Solar ya Djibouti katika mchezo wa kirafiki ambao kwa mara ya kwanza beki wa zamani wa Yanga, Djuma Shabani aliitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya kukwama kusajiliwa katika dakika za mwisho za dirisha la usajili lililofungwa Agosti 31.

Sasa habari zilizopo ni kwamba, tayari pande zote mbili zimeshakubaliana zikisubiria dirisha dogo, lakini kazi ikiachwa mikononi mwa kocha mkuu Youssouph Dabo ili kumsoma kwa sasa ndani ya kikosi hicho na kuchagua mchezaji gani wa kumchomoa ili beki huyo Mkongomani achukue nafasi kulingana na kanuni.

Chanzo changu makini kimenidokeza kuwa mastaa waliokalia kuti kavu ni kipa Ali Ahamada aliyetakiwa kumpisha Djuma ila aligoma baada ya kudai viongozi walichelewa kumpa taarifa hizo.

Mbali na Ahamada, kipa mwingine Mghana Abdulai Iddrisu huenda pia akaachwa kutokana na kile kinachoelezwa kutokuwa kwenye maelewano mazuri na kocha wake wa makipa, Khalifa Ababakar Fall.

Endapo Iddrisu ataachwa itatoa nafasi kwa kipa Mnigeria, John Noble anayekipiga kikosi cha Kitayosce kusajiliwa kwani viongozi wa timu zote mbili wamewasiliana juu ya upatikanaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live