Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma Shabani atangaza vita mpya

Djuma Shaban Nnn Djuma Shabani

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kulia wa Yanga, Djuma Shabani, amesema kuwa licha ya kuibuka na ushindi katika michezo miwili mfululizo ya ligi kuu, lakini kuna ugumu mkubwa sana katika ligi ya msimu huu, jambo ambalo wanatakiwa kujipanga kuhakikisha wanapambana kupata ushindi katika kila mchezo.

Djuma tangu asajiliwe na Yanga akitokea AS Vita ya nchini DR Congo, amekuwa mchezaji tegemeo ndani ya klabu hiyo akitumika kama beki wa kulia.

Djuma alisema kuwa msimu huu unaonekana kuwa mgumu zaidi ya msimu uliomalizika kutokana na timu nyingi kusajili wachezaji bora huku wakihitaji kupata matokeo mazuri mbele ya bingwa mtetezi, jambo ambalo kwao wanatakiwa kupambana kushinda zaidi japokuwa wameanza vyema.

“Ni kweli tumeanza kwa kupata ushindi katika michezo miwili mfululizo lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata kwa kuwa tunakwenda kukabiliana na michezo migumu.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu kwa kuwa timu nyingi zimefanya usajili wa maana na zote zinahitaji kupata matokeo mazuri mbele yetu kwa kuwa msimu uliopita tulifanikiwa kuwa mabingwa, hivyo ili tuweze kuendelea kushinda basi tunatakiwa katika kila mchezo kuweka nguvu ya ziada ili tufanikiwe kuwa mabingwa,” alisema beki huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live