Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djuma Shaban aachwa Dar

Djuma Shaban Fr Djuma Shaban

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kitasa wa Yanga, Djuma Shabani 'Soda ya Bemba' amebaki nchini Tanzania wakati kikosi cha wachezaji wenzake kikiondoka kuelekea Tunisia leo, Ijumaa Novemba 4, 2022 mchana.

Djuma Shabani amelazimika kubaki Tanzania akiuguza majeraha ya nyama za paja aliyoumia wakati akiwa mazoezini.

Yanaga wanakwenda Tunisia kutupa karata yao ya mwisho katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ili kutafuta nafasi ya kufuzu katika hatua ya makundi ya ligi hiyo baada ya kuondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Hilal ya Sudan Kaskazini.

Yanaga atacheza mchezo wake Novemba 9, dhidi ya Club Africain ya Tunisia huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoa sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 3, kwenye Dimba la Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live