Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djigui Diarra, kitabu cha mafundisho kwa Makipa Ligi Kuu

Djugui Diarra Keeper Mlinda Mlango wa Yanga, Djigui Diarra

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aina ya uchezaji wa kipa wa Yanga, Djigui Diarra ni kama somo kwa wazawa wanaocheza nafasi hiyo, kujifunza utulivu wake na namna anavyoweza kutumia miguu yake kuichezesha timu nje na kuzuia.

Miongoni mwa makipa hao ni Metacha Mnata aliyekiri uwezo wa Diarra unamsaidia kuongeza thamani ya nafasi anayopata kucheza, kwani tangu alirejee ndani ya kikosi hicho kupitia dirisha dogo alidaka dhidi Rhino Rangers waliyoichapa mabao 7-0 mchezo wa ASFC uliopigwa Januari 29, Benjamin Mkapa.

Metacha alisema “Diarra kiufundi anatoa somo, kwani ni mtulivu, anaweza akatumia miguu kushirikiana na wachezaji wa ndani kupigiana pasi kwa kujiamini;

“Kucheza naye timu moja, kwangu kunanifanya ninapopata nafasi ya kucheza kuitumia kwa umakini nikijua kuna ushindani mkali pia yapo mambo ambayo kiufundi najifunza, kwani kujifunza siyo dhambi.”

Alisema hana maana kwamba makipa wenzake wazawa ni wabaya, isipokuwa anaiangalia chachu ya ushindani aliyoileta Diarra ambayo haoni ubaya kumpa sifa zake kwa kitu anachokiona anakifanya kwa ubora.

Kipa wa Ruvu Shooting, Isihaka Hakimu alisema “Diarra nje na ulinzi anajiongeza kwenye majukumu mengine, mfano kipa anapopanda kusaidia mashambulizi inaondoa hali ya kujiamini kwa wapinzani wanaocheza nao.”

Kwa upande wa kipa wa Prisons, Mussa Mbisa alikiri Diarra anajiamini; “Kama kipa wa kigeni ameonyesha kitu cha tofauti, pia anajitahidi kuwasoma wapinzani kuanzia mbali ndio maana ni mgumu kumfunga, kwani tayari anakuwa amejipanga na kujiandaa namna ya kuondoa hatari.”

Diarra anaongoza kwa klinishiti 13 kabla ya mchezo wao wa juzi Jumatano dhidi ya KMC, pia ndiye aliyeondoa ufalme wa Aishi Manula akichukua kipa bora msimu uliopita.

Makipa wa zamani nao hawakuwa nyuma kutoa mitazamo yao namna wanavyomuona Diarra, alianza kocha wa makipa wa Ihefu, Manyika Peter aliyesema “Ni kipa mzuri ila haimanishi wazawa hawapo wenye uwezo kama wake aliowataka waongeze kujiamini zaidi .”

Kocha wa zamani wa Simba, Idd Pazi alisema kwa soka la kisasa linahitaji kipa anayejiongeza ili kujitafutia ulfame wake

“Kila wakati napenda kumtolea mfano Juma Kaseja ambaye mazoezi binafsi na roho yake ya kutoridhika ilimfanya awe mfano kwa wengi waliokuja nyuma yake.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live