Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djigui Diarra atua na mbinu mpya Yanga

Diarra Lawama Djigui Diarra atua na mbinu mpya Yanga

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa makipa wa Yanga, Alaa Meskini amesema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, zimemuongezea ubora Djigui Diarra huku akidai kwamba nyanda huyo ametua nchini akiwa na mbinu mpya ambazo anaamini zitakuwa chachu ya timu hiyo kutetea taji pamoja na kuingia na nguvu mpya kimataifa.

Diarra alicheza mechi zote za Afcon katika timu ya Taifa ya Mali mpaka ilipotolewa hatua ya robo fainali dhidi ya Ivory Coast. Ipo hivi; Licha ya kuamini kuwa Diarra ataibeba Yanga akiwa langoni kuhakikisha analinda lango pia amewataka Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery kukubali kuzidiwa uwezo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meskini alisema ubora alioondoka nao ndani ya kikosi cha Yanga akaenda zake Afcon umeongeza vitu vingine vya ziada na ni vizuri zaidi kwake, na kama kocha lakini pia amewataka washindani wake kumtumia kama darasa.

“Yanga ina kipa bora ambaye ana kila kitu. Anajua kuanzisha mashambulizi na ana nguvu za mikono akirusha (mpira) ni kama amepiga. Kama mwalimu najivunia kufundisha wachezaji wa aina yake. Diarra amerudi na mambo mengi sana bora,” alisema.

“Nina makipa watatu nawaangalia kwa ukaribu na ndio waliobeba matarajio ya wana Yanga kuhakikisha wanatetea taji la ligi. Kuna Metacha na Mshery wote wanapambana kuwa bora na hili linawezekana kama kila mmoja atakubali kuwa kuna aliye bora zaidi yake.”

Meskini alisema: “Na-weza kusema Diarra ni miongoni mwa makipa bora zaidi ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa na hili linathibitishwa na kuitwa kwake kwenye kikosi cha timu ya Taifa kubwa kama Mali ambayo pia imethibitisha hilo kwa kumpa nafasi kwenye mechi zote akidaka kwa ubora.”

Aliongeza kuwa kina Diarra kuishia robo fainali ya Afcon ni sehemu ya mchezo lakini haiondoi ubora aliouonyesha mbele ya makipa wakubwa waliokuwa wanamuweka benchi miaka ya hivi karibuni ndani ya timu ya Mali.

“Nafurahi amerejea na vitu vingi vipya na vikubwa. Naamini kwa nafasi yake na namna ambavyo amecheza anarudi kuendeleza ubora wake na ndiye atakuwa msaada mkubwa kwa timu kutetea taji ambalo kwa upande wangu naamini linabaki tena Yanga.” alisema.

Katika mechi walizocheza Yanga, Diarra amedaka tisa akikosekana kwenye michezo minne kati ya hiyo tisa aliyodaka ana ‘clean sheet’ sita.

Akiwa na timu ya taifa ya Mali, Diarra amecheza mechi nne dakika 90 huku akiruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili dhidi ya Tunisia pale walipotoka sare ya bao 1-1 na dhidi ya Burkina Faso katika ushindi wao wa mabao 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live