Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dirisha la usajili limefunguliwa, Vilabu hivi vyapigwa 'Stop' kufanya usajili

Injinia Hersiiii Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa orodha ya vilabu vya Ligi Kuu bara ambavyo vimefungiwa kusajili na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na TFF mpaka zitakapowalipa wachezaji

Taarifa ya TFF ya leo Juni 18, 2024 imevikumbusha vilabu vyote kuwa Dirisha la usajili msimu wa 2024/2025 kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), NBC Championship (NBCCL), First League (FL) na Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) limefunguliwa Juni 15, 2024 lakini vilabu ya Young Africans, Singida Fountain Gate FC, Tabora United FC, Biashara United FC na FGA Talents FC vimefungiwa KUSAJILI

“Klabu ambayo itawalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili. Hadi leo asubuhi kupitia mfumo wa FIFA (FIFA legal portal) hakuna taarifa ya klabu yoyote kati ya hizo iliyowalipa wahusika.” — TFF

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: