Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Diogo Jota huenda akakosa mchezo wa fainali ya Carabao Cup kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Milan.
Diogo Jota alitolewa nje kipindi cha kwanza pale ambapo alipata majera ya ankle, na alipoulizwa kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp kuhusu hali ya mshambuliaji huyo, baada ya mchezo kuisha alisema, “haionekani kuwa amepata majeraha makubwa”
Baada ya kufanyiwa vipimo na kuangaliwa tatizo imeonekana ana matatizo ambayo tofauti na ilvyotarajiwa, na mshambuliaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwenye mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Norwich, na bado kuna wasiwasi kama ataweza pona mpaka siku ya mchezo wa fainali dhidi ya Chelsea.
Mchezo wa fainali utachezwa baada ya siku 10 kuanzia sasa, na bado hakuna uhakika kama mshambuliaji kinara wa kufunga ambaye anashika namba mbili kwenye klabu hiyo atakuwa sawa.