Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dilunga atoa neno Msimbazi kuelekea mechi zijazo

Hassan Dilunga Hd (600 X 400) Hassan Dilunga "HD"

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa Simba Hassan Dilunga "HD" amewaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuisapoti timu huku wao kama wachezaji wakiahidi kuwapa furaha.

Dilunga amesema baada ya kipindi kigumu kupita cha kushindwa kupata matokeo upepo umeanza kurejea na siku za furaha zitarudi tena kama kawaida.

Dilunga amesema kuwa amefurahi kuwepo katika kikosi kilichoibuka na ushiundi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Dar City na anaamini wataendelea kushinda kuanzia wakati huu.

Katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora dhidi ya Ruvu Shooting, Dilunga amesema wanajipanga kuhakikisha wanashinda na lengo ni kutetea Ubingwa.

"Nimefurahi kuwa sehemu ya Kikosi kilichopata ushindi baada ya kupitia kipindi kigumu, Mashabiki wetu waendelee kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti na sisi tutawapa furaha"

"Sisi ni mabingwa watetezi wa michuano hii, tunaenda kukutana na Ruvu Shooting tutahakikisha tunashinda ili tuvuke hatua inayofuata na hatimaye tutetee taji letu" amesema Dilunga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live