Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dili la Msuva Saudi Arabia lipo hivi

Smsuva27 1692777281380.jpeg Dili la Msuva Saudi Arabia lipo hivi

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Saimon Msuva amekiri kumalizana na Alnajmah FC ya Saudi Arabia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa mkataba wa miezi sita.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu akiwa Ivory Coast, Msuva amesema ni kweli amemalizana na timu hiyo kwa mkataba wa muda huo.

"Nakwenda kucheza nchi ambayo tayari nina uzoefu nayo, sioni shida yotote itakayonisumbua. Kilichobadilika ni timu tu, natumaini nitafanya kile kitakachonipeleka kwa usahihi," amsema mshambuliaji huyo mwenye bao moja katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) zinazoendelea nchini humo.

"Kuhusina na kusaini mkataba kwa muda mfupi hiyo ni mipango ambayo ipo sasa. Kitakachofuata tumuachie Mungu, sasa tuzungumze dili lililokamilika."

Msuva amesema anafurahi kupata timu katika muda wa dirisha na anafurahia hilo, lakini mambo mengi yalikuwa yanazungumza sasa ni muda wake wa kufanya kazi mara baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa.

Kutua kwake Alnajmah FC atakuwa ametimiza timu tano nje ya nchi tangu alipoondoka Yanga msimu wa 2017-18 akipita katika timu za Difaa El Jadida na Wydad Casablanca za Morocco, Al Qadsiah ya Saudia Arabia na JS Kabylie ya Algeria.

Chanzo: Mwanaspoti