Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dili la Madeleke, Pamba limetiki

Samson Madelekaaaa Samson Madeleke

Sun, 7 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Pamba Jiji imekamilisha uhamisho wa aliyekuwa beki wa kulia wa Mashujaa, Samson Madeleke kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zimeliambia Mwanaspoti kuwa Madeleke amekamilisha uhamisho baada ya kutofikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya na Mashujaa kufuatia ule wa miezi sita aliousaini kuisha msimu uliopita.

“Ni kweli nyota huyo amesajiliwa na Pamba kama mchezaji huru baada ya mkataba aliokuwa nao na Mashujaa kumalizika na muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa kikosini. Wapo na wengine ambao tunaendelea kufanya mawasiliano nao,” kilisema chanzo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Pamba, Bhiku Kotecha alisema kwa sasa kinachoendelea ni vikao vya ndani na kila kitu kitakapokamilika wataweka wazi akisisitiza mashabiki wa kikosi hicho watarajie mambo mazuri.

“Tumefanya uhamisho kwa kuzingatia matakwa ya benchi la ufundi. Kujua ni nani na nani wameingia tutaanza kuwatambulisha siku yoyote kuanzia sasa. Hilo linakuja baada ya kuwaongezea wachezaji walioipandisha timu mikataba mipya,” alisema.

Samson alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema muda muafaka utakapofika ataweka wazi juu ya timu atakayoichezea msimu ujao.

Madeleke ameachana na Mashujaa baada ya kuitumikia kwa miezi sita tangu alipojiunga nayo Januari, mwaka huu akitokea Mbeya City, huku akiwa ni mchezaji wa pili kujiunga na Pamba Jiji baada ya mshambuliaji, Frank Ng’amba kutokea TMA FC.

Chanzo: Mwanaspoti