Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dili la Labota lachukua sura mpya Yanga

Manu Labota Bola Dili la Labota lachukua sura mpya Yanga

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ukisikia umafia, ndio huu. Yanga ilikuwa ikimpigia hesabu winga Mkongomani, Manu Labota Bola, lakini kabla haijamalizana naye, dili likatibuka na jamaa akaibukia Singida Fountain Gate.

Mabosi wa Yanga wakasikitika kwa kumkosa mchezaji huyo na kuendelea na yao, lakini wakati kila mmoja akiamini Labota keshatua Singida kwenda kuliamsha mambo yamebadilika baada ya mchezaji huyo kutua Ihefu kama masihara vile.

Ipo hivi. Winga huyo tayari yupo nchini tangu juzi, lakini akiwa ni mchezaji wa Ihefu iliyopokutisha baadhi ya mastaa iliyokuwa nao kutokana kilichoelezwa timu ipo mbioni kuuzwa kwa mmoja vigogo nchini.

Wachezaji wengi wa timu hiyo wameomba kuondoka kwa hiyari yao, huku wengine wakiachwa kimya kimya kupitia dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa Jumatatu, huku mmoja ya wachezaji wapya alitua ili kuimarisha kikosi hicho akiwa ni Labota.

Baada ya dili la kwenda Yanga kuyeyuka, Mwanaspoti liliripoti kuwa Singida ilikuwa katika hatua za mwisho kumalizana na Labota kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, lakini ghafla mambo yamebadilika.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ya Ihefu FC, winga huyo wamemnyakua muda mchache baada ya kutua Dar es Salaam na kumficha kwenye moja ya hoteli iliyopo jijini.

“Suala na Labota kusajiliwa na Singida sisi hatulifahamu tunachotambua sasa huyo ni mchezaji wa Ihefu baada ya mazungumzo ya pande zote mbili kwenda sawa na yupo jijini, muda ukifika atatambulishwa na timu yetu,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake litajwe.

Winga huyo ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya FC Lupopo utakuwa ni usajili wa kwanza kwa Ihefu FC endapo dili lao litakamilika kama wao walivyosema.

Wakati winga huyo akitajwa timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha, Mecky Maxime tayari imeachana na Nassoro Saadun, beki mkongwe Juma Nyosso, Rashid Juma, Charles Ilanfya.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: