Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job atoboa ulipo ubora wa Yanga

DICKSON JOB 2 Beki wa Yanga, Dickson Job(kulia) na Eng. Hersi

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Mlinzi wa kati wa Yanga, Dickson Job amefunguka kwa kutamba kuwa, Yanga ya sasa ina viungo bora na wazoefu jambo ambalo linalowafanya wawe na timu imara na kuanza vema kwa kushika usukani wa Ligi kuu ya NBC Tanzania 2021-22.

Job anayecheza sambamba na nahodha wake, Bakari Mwamnyeto kwenye pacha ya walinzi wa kati amesema, viungo wao wakabaji walio bora, Yannick Bangala na Khalid Aucho wamewafanya wasiwe na kazi kubwa ya kulinda lango lao na kumsaidia kipa wao Djigui Diarra asifikike kirrahisi.

Beki huyo kitasa amesema: “Tunacheza na walimu kiwanjani. Ukiachana na kocha Nabi, tumeongezewa nguvu kubwa ambayo imekuwa na msaada kwetu. Hatufanyi makosa ya kizembe ndiyo maana unaona tulivyo imara katika Ulinzi”.

Yanga kwa sasa inaongoza Ligi kuu ya NBC Tanzania kwa kuwa na alama 15, ushindi wa asilimia mia katika michezo yake mitano wakiwa vinara wa ufungaji wakiwa na mabao 9 na kuruhusu kufungwa bao moja pekee.

Na kwenye michezo hiyo, Dickson Job amecheza michezo yote, mara moja akicheza na Yannick Bangala na mara nne na Bakari Mwamnyeto kwenye eneo la ulinzi.

Chanzo: eatv.tv