Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job: Sio kitu rahisi kuondoka Yanga

Dicson Job Dickson Job

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Furaha kwa mashabiki wa Yanga ni kuona beki wao, Dickson Job kuendelea kusalia kwa miaka miwili mbele baada ya kusaini mkataba wa kuhudumu kwenye timu hiyo.

Job alikuwa anahusishwa na kujiunga Simba, huku ikitajwa pia kuwa na dili zingine nje ya nchi, lakini Yanga wametoa picha za mchezaji huyo kusaini miaka miwili ikiwa ni siku moja tangu Mwanaspoti ilipofichua beki huyo ameamua kusaini mkataba mpya wa kubaki Jangwani.

Akizungumza Dickson alisema ilikuwa lazima kwake kubaki Yanga kwani ni timu ambayo amekuwa nayo kwenye wakati mzuri, pia imempa kile ambacho amekihitaji.

"Kikubwa ni kuwashukuru viongozi na mashabiki wote wa Yanga kwa kuniamini na kuamua kuniongezea mkataba, nami kama mchezaji na nitaendelea kuipambania nembo kila ninapopata nafasi," alisema Job aliyesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar.

Tangu aliposajiliwa, beki huyo wa kati amekuwa katika kiwango kizuri ndani ya miaka miwili huku akiwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na huku akibadilishana nafasi na nyota wengine wa nafasi hiyo kikosini akiwamo nahodha Bakar Mwamnyeto, Yannick Bangala, Ibrahim Abdullah 'Bacca' pamoja, huku Shaibu Abdallah 'Ninja' na Mamadou Doumbia wakikosa nafasi kikosi cha kwanza.

Job mwenye bao moja katika Ligi Kuu Bara alikuwa kwenye sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ambayo inacheza michuano ya Kombe la Mataifa kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) na kwenye mechi za hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Chanzo: Mwanaspoti