Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job: Sijawahi kujutia kimo changu

Mwamnyeto Job Kibwana Dickson Job: Sijawahi kujutia kimo changu

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Taifastars na baadhi ya wachambuzi walisema kwa kimo chako hupaswi kucheza beki wa kati, ulishawahi kujutia kuhusu kimo na nafasi unayocheza?

"Hata siku moja kwenye maisha yangu ya soka sijawahi kujutia kimo changu, mimi naamini mipira ya juu ni timing tu, wapo mabeki warefu sana lakini wanafungwa magoli ya kichwa.

"Katika msimu huu sidhani hata yanafika magoli (3) ya kichwa tuliyofungwa nikiwa beki wa kati, sikumbuki. Beki yetu ndiyo iliyoruhusu magoli machache zaidi ligi kuu," amesema Dickson Job.

Kucheza timu kubwa Kama Yanga kuna presha unayoipata ukizingatia ulitoka kwenye timu ndogo?

"Yeah, ni kweli kucheza timu kubwa kama Yanga kuna presha ambayo huwezi kuipata kwenye timu ndogo, presha hiyo sio kwa wachezaji tu hata kwa viongozi na makocha.

"Yanga ni timu inayotaka kushinda kila mechi ili kupata Ubingwa kwa hiyo kila mechi ni muhimu. Tumetwaa Ubingwa msimu huu lakini tayari tunapaswa kushinda Ubingwa msimu ujao na misimu mingine. Hiyo ndio maana ya timu kubwa," amesema Dickson Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live