Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job: Mtuombee, bado tunayo nafasi ya kufanya vizuri

Sad Job Yanga Dickson Job: Mtuombee, bado tunayo nafasi ya kufanya vizuri

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Yanga SC, Dickson Job amewomba mashabiki na wapenzi wa klabu yao, kuwaombea dua kwani bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Job ametoa kauli hiyo leo Desemba 5, 2023 walipokuwa njiani kuelekea nchini Ghana kuwafata Medeama.

"Mashabiki watuombee, bado tunayo nafasi ya kufanya vizuri katika michezo iliyosalia, tutakwenda kupambana ili tupate matokeo," alisema Job.

Yanga wamesaliwa na michezo minne ya Makundi baada ya kucheza miwili ambapo wamepoteza mmoja 3-0 dhidi ya CR Beloizdad na mwingine wamepata sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly.

Kwenye kundi lao, Yanga ndio wanaoshika mkia huku kundi lao likiongozwa na Al Ahly mwenye alama 4 sawa na CR Beloizdad. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Medeama ambao wana alama 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live