Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diatta ajiweka mtegoni CAF

Krepin Diatta Winga wa Senegal, Krepin Diatta

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Senegal, Krepin Diatta huenda akakumbana na adhabu kali kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kulituhumu kula rushwa kufuatia mabingwa hao watetezi wa Afrika kutupwa nje kwa mikwaju ya penalti mbele ya Ivory Coast kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora katika fainali za Afcon 2023, Jumatatu iliyopita.

“Mmetuua. Mmekula rushwa. Kaeni na kombe lenu,” alisema winga Diatta, anayekipiga kwenye klabu ya AS Monaco alipokuwa akiwashambulia viongozi wa Caf mjini Yamoussoukro.

Ivory Coast ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya bao 1-1, huku Senegal wakiendeleza rekodi ya kumshuhudia bingwa mtetezi akishindwa kutetea taji la Afcon 2023, ambapo hakuna timu nyingine iliyowahi kufanya hivyo tangu Misri iliponasa taji kwa mara tatu mfululizo mwaka 2010.

Diatta alikasirika kwa sababu Senegal hakuipewa penalti mapema kwenye kipindi cha pili wakati Ismaila Sarr alipoangushwa ndano ya boksi kwa kubanwa miguu na beki wa Ivory Coast, Odilon Kossounou.

Senegal iliongoza 1-0 kwa bao la mapema la Habib Diallo, lakini refa wa Gabon, Pierre Ghislain Atcho hakuamuru ipigwe penalti wala kwenda kwenye skrini ya VAR kutazama marudio ya rafu aliyochezewa Ismaila Sarr ndani ya boksi la Ivory Coast, ambao ni wenyeji wa fainali hizo za Afcon 2023.

Chanzo: Mwanaspoti