Wananchi wanatoka vichwa chini Highland Estates. Kwa mara nyingine tena highland Estates uwanja mgumu kwa Wananchi, wanadondosha alama tatu kama ilivyokua msimu uliopita.
Yangasc walifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao ili kuwapa nafasi wachezaji wengi ambao wamekua hawapati nafasi ya kuanza mara nyingi, Skudu, Mauya, Sureboy, Kibabage, Kibwana huku wakicheza mfumo wao mama 4-2-3-1, wakiwa na mlengo na kucheza pasi nyingi kupitia katikati ya uwanja huku pia wakinufaika na winga wao asilia Skudu na Moloko.
Goli la Mapema la Pacome Zouzoua, liliwatoa usingizini Ihefu, wakaweka presha kubwa kwenye mpira, kwa idadi kubwa ya viungo, huku wakiwanyima nafasi Yanga kumiliki mpira, wakafanikiwa kupata goli la kusawazisha kwa mpira wa kutengwa.
Mabadiliko ya Yanga kipindi cha pili, Max, Aucho, na Aziz Ki ilikua ni kuongeza idadi ya watu katikati na ubunifu eneo la mwisho wakiwa na uchu wa kutafuta bao, Ihefu wakaweka mtegao wa transition ya haraka kila wakitoka nyuma kwa mashambulizi ya kushtukiza, ni umakini tu ulikosekana wangepata zaidi ya zile goli mbili.
Note: Baada ya goli la pili, Yanga walitoka mchezoni, walikua slow sana, kwenye matukio mengi, walicheza mfumo ambao walinzi wa ihefu wali-enjoy zaidi mipira mirefu.
Charles Ilamfya, what a goal what a move!! Alikuwa na siku nzuri sana alifanya alichokitaka. Skudu ana mambo mengi ya kuboresha hasa kutoa mpira mapema mguuni.
Goli la kwanza la Ihefu, Diarra hawezi kukwepa lawama, alikuwa na chaguo bora zaidi kuutoa mpira kwa mkono mmoja na sio alivyofanya.