Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra azidi kuandika rekodi CAF

Diarra 01 E1664965062636 1170x650 Djigui Diarra.

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa kikosi cha Yanga Sc, Djigui Diarra, juzi alifanikiwa kucheza mchezo wake wa kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini ambao Mali walichomoza na ushindi wa magoli 4-0.

Hii ilikuwa mechi ya pili kwa Diarra kucheza akiwa na Timu ya Taifa ya Mali na kutoka na Cleansheets, akiisaidia timu yake hiyo kufuzu michuano ya AFCON itakayofanyika mwaka 2024 nchini Ivory Coast.

Diarra ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa nchini Mali. Akiwa na klabu yake ya Stade Malien, alibeba mataji kadhaa ikiwemo Ligi Kuu Mali (5), Kombe la FA (3) na Malian Super Cup (2).

Kwa upande wa Timu ya Taifa, amekuwa na rekodi bora na pengine kubwa zaidi katika historia ya taifa lao, kwani akiwa kipa namba moja aliifikisha Mali Fainali ya CHAN mara mbili, 2016 na 2021.

Mwaka 2016 alifungwa fainali na DR Congo, akatajwa kuwa kipa namba mbili wa Afrika kwa ngazi ya Taifa kwa wachezaji wa ndani baada ya kudaka penalti 3 katika mechi 6.

Mwaka 2020, akafungwa fainali ya CHAN dhidi ya Morocco, akiweka rekodi ya kucheza dakika 365 bila kuruhusu goli ikiwemo kudaka penalti muhimu hatua ya nusu fainali dhidi ya Guinea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: