Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra avunja rekodi Mali

Djigui Diarra Maliii Djigui Diarra

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra amecheza dakika 90 timu yake ya taifa ya Mali ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wao wa kwanza kundi E wa fainali za Afcon 2023 zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Huo ni mwendelezo mzuri kwa mastaa wa Yanga, baada ya jana Aziz Ki timu yake ya Burkina Faso kushinda bao 1-0 dhidi ya Mauritania, Aziz Ki akicheza dakika 87.

Kwenye mchezo huo ambao Diarra alionekana kuwa bora eneo lake la ulinzi ambalo alipigiwa mashuti 12 langoni kwake, sita yalilenga goli na matano yalitoka huku moja likizuiliwa.

Kati ya mashuti hayo sita aliokoa mipira ya hatari mitano ambayo kama sio ubora wake basi timu yake ingefungwa idadi ya mabao hayo.

Licha ya timu yake kumaliza kwa umiliki mdogo wa kuchezea mpira wakiwa na asilimia 45 kwa 55 lakini waliibuka na ushindi wa mabao hayo.

Timu hizo ziligawana vipindi kwani Afrika Kusini wao walifanya mashambulizi mengi zaidi kipindi cha kwanza ambacho kiliisha kwa suluhu ya bila kufungana.

Kipindi cha pili, Mali walirudi kwa nguvu wakitumia dakika sita kufunga mabao mawili yaliyowapa uongozi hadi mechi ilipoisha, bao la kwanza lilifungwa dakika ya 60 na Traore na la pili dakika ya 66 likifungwa na Sinayoko.

Baada ya ushindi huo, Mali wamevunja rekodi ya kucheza mechi 55 za Afcon bila kushinda mchezo wowote hivyo Diarra ameingia kwenye rekodi ya kuwa kipa aliyesimama langoni akiwa na timu iliyofunga mechi baada ya michezo hiyo.

Kundi E ambalo linaongozwa na Mali, Namibia wote wana pointi tatu tofauti ni idadi ya mabao ya kufunga, Tunisia wanashika nafasi ya tatu wakati Afrika Kusini wanaburuza mkia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live