Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa NIC

Kibabage Bacca Diarra Diarra ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa NIC

Sat, 6 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja wa timu ya Yanga, amefanikiwa kushinda Tuzo ya NIC Insurance baada ya kuibuka Mchezaji Bora wa Mwezi Desemba ndani ya kikosi hicho.

Diarra ameshinda tuzo hiyo inayotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya kuwashinda Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ na Nickson Kibabage alioingia nao fainali.

Mashabiki na wanachama wa Yanga SC, ndio wameamua ushindi huo kwa Diarra baada ya kupiga kura kupitia application ya Yanga SC.

Katika kura hizo, Diarra amepata asilimia 60, ⁠Ibrahim Bacca 25% na ⁠Nickson Kibabage 15%.

Tuzo hizo zilianza kutolewa mwezi Oktoba 2023 chini ya udhamini wa NIC, ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Stephane Aziz Ki, kisha Pacome Zouzoua akashinda mwezi Novemba.

Baada ya kuibuka mshindi, Diarra anatarajiwa kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live