Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra arejea rasmi kikosini, Yanga yashusha presha

Diarra 01 E1664965062636 1170x650 Diarra arejea rasmi kikosini Yanga

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwa na majukumu kwenye timu yake ya Taifa ya Mali iliyokuwa ikishiriki michuano ya AFCON nchini Ivory Coast, kipa wa Yanga SC, Djigui Diarra rasmi amerejea kikosini.

Diarra katika michuano hiyo ya AFCON ambayo Mali iliishia hatua ya robo fainali, alicheza mechi zote tano, tatu hatua ya makundi, hatua ya 16 bora na robo fainali.

Baada ya kurejea, Diarra anatarajiwa kufanya mazoezi na wenzake leo Jumanne ambapo kikosi hicho kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Avic Town kuanzia saa 10:00 jioni.

Mazoezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao wa ugenini katika Ligi Kuu ya NBC mzunguko wa pili dhidi ya KMC utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii Februari 17, 2024 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: