Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra anarudi lini? Yanga wafunguka

Diarra 01 E1664965062636 1170x650 Golikipa wa Yanga, Djigui Diarra

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa klabu ya Yanga, Djigui Diarra anatarajia kujiunga na timu hiyo Alhamisi baada ya kukamilisha majukumu yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Mali.

Diarra ambaye aliwaachia msala makipa wawili wa timu hiyo Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery anarudi tayari kwa ajili ya kuendelea na mikiki mikiki ya kutetea taji wanalolishikilia la Ligi Kuu Bara.

"Diarra atakuja nchini keshokutwa Alhamisi, kila kitu kipo tayari na siku hiyohiyo ataungana na wenzake kambini, nasikia wengine wanasema sijui ana dili huku na kule, lakini ninachofahamu ni kwamba kila kitu kitafanyika akiwa hapa nchini," kilisema chanzo.

Ipo hivi; Baada ya Diarra kukosekana kwenye mechi tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Yanga ikishinda 5-1 na mechi mbili za ligi dhidi ya Kagera Sugar wakitoka suluhu na dhidi ya Dodoma Jiji jana wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 kocha wa Yanga Miguel Gamondi alionekana kukosa mbadala sahihi.

Hii ni baada ya mechi tatu kutumia makipa wawili tofauti akitoa nafasi kwa wote wawili mmoja akitumika kwa dakika 90 bila kuruhusu bao na mwingine kacheza dakikia 180 akiruhusu bao moja na kuipa timu pointi zote tatu.

Mchezo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), alimtumia Mshery ambaye aliruhusu bao moja timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1, mchezo uliofuata wa ligi alimtumia Metacha ambaye hakuruhusu bao mchezo ukiisha kwa suluhu ambaye alitumika tena kwenye mchezo dhidi ya Dodoma.

Diarra kwenye mechi 11, walizocheza Yanga kwenye ligi amedaka mechi tisa akikosekana kwenye michezo miwili, kati ya hiyo aliyodaka sita hakuruhusu lango lake litikiswe.

Akiwa na timu yake ya taifa ya Mali kwenye michuano ya Afcon 2023, Diara amecheza mechi nne zote dakika 90, akiruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili dhidi ya Tunisia wakitoka sare ya bao 1-1 na dhidi ya Burkina Faso 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: