Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra anarudi Mahala pake, hamasa ya kutosha Jangwani

Diarra Golikipa wa Yanga, Diarra Djigui

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango namba moja wa Yanga, Djigui Diarra baada ya kukosekana kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara sasa anatarajia kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi itakayopigwa Februari 23 kwenye Uwanja wa Manungu sambamba na beki Djuma Shaban.

Diarra aliyekuwa nje ya uwanja kutokana na kujumuishwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Mali, amerejea nchini baada ya timu yake kutolewa huku Djuma alikuwa akitumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu kutokana na kumfanyia mchezaji mwenzake mchezo usio wa kiungwana.

Wakati mpango wa wawili hao kurudi uwanjani umeiva, kipa namba mbili aliyekuwa anaibeba Yanga wakati Diarra yupo Afcon, Aboutwalib Mshery anatarajia kucheza mechi yake ya mwisho Februari 15, wakati Yanga itakapoivaa Biashara United katika mechi ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

Mshery ambaye amedaka mechi nne hadi sasa za Ligi Kuu ambazo ni sawa na dakika 360 bila kuruhusu bao, anatarajia kumalizia dakika 90 za mwisho kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Jumanne ijayo dhidi ya Biashara United.

Chanzo cha ndani ya timu hiyo kililiambia Mwanaspoti, kuwa Mshery ni mgonjwa na kwa mechi kadhaa amekuwa akicheza na maumivu lakini ni mpambanaji na aliomba acheze mechi ya Mbeya City na Biashara United ambayo ni ya shirikisho ili kuondoa maneno kwa mashabiki na wadau wa soka kwamba ameanza kukosa nafasi baada ya Diarra kurudi.

“Mshery anaumwa lakini ni mpambanaji na alikuwa akicheza na maumivu ndio maana aliomba aendelee kuonyesha ubora wake dhidi ya Mbeya City na Biashara Februari 15 na baada ya hapo langoni atakaa Diarra wakati kipa namba mbili anaendelea kujiuguza na kupata mapumziko kwa muda,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta daktari wa timu, Dk Shecky Mngazija ambaye alithibitisha kipa huyo kupata tatizo ambalo aliliweka wazi kuwa halikuwa kubwa wamelifanyia kazi haraka na ndio maana alionekana uwanjani.

“Yanga ina majeruhi kama Kibwana Shomari, Yacouba Sogne na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao wapo chini ya daktari wa viungo. Mshery alicheza dhidi ya Mbeya City leo mnauliza hali yake, inakuwaje mgonjwa apewe nafasi ya kucheza?” alihoji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live