Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra ana kazi ngumu Yanga

Diarra Pic Data Golikipa wa Yanga Djugui Diarra

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga ni Djigui Diarra. Taarifa ya daktari wa timu hiyo imethibitisha kipa namba mbili Aboutwalib Mshery atakaa nje ya uwanja mwezi mzima kutokana na kusumbuliwa na goti.

Yanga ambayo imemaliza kinara mzunguko wa kwanza na pointi 38, itamkosa Mshery kwa wiki nne tangu aonekane kwenye benchi kwa mara ya mwisho dhidi ya Ihefu ambapo walipasuka mabao 2-1.

Akizungumza Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema Mshery hatakuwa kwenye programu kwa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na goti.

“Ni kweli Mshery ni majeruhi, lakini haiondoi timu kuendeleza ushindani na kufikia malengo, kuna Diarra na Erick Johora ambaye ni mechi tatu au nne mfululizo amekuwa benchi,” alisema.

“Tunatambua umuhimu wake, ila afya pia ni muhimu atakuwa nje ya timu akifanyiwa matibabu na tunamtakia matibabu mema ili arudi akiwa fiti na kuisaidia timu kufikia malengo. Kila mmoja ana umuhimu wake kwa wakati, hivyo kukosekana kwake ni nafasi kwa wengine kuonyesha uwezo.”

Walter alisema timu iko kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Jumapili itakapovaana na Kurugenzi ya Simiyu.

Alisema mbali na Mshery, mshambuliaji Heritier Makambo anaendelea kujiuguza na atakosekana kikosini ila wengine wote wapo fiti ni suala la kocha kuamua kumtumia nani lengo likiwa ni kuonyesha ushindani kwa wapinzani wao.

Mshery amekosekana kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania na Namungo na ataendelea kutokuwa sehemu ya kikosi hadi matibabu yake yatakapokamilika huku Diarra akisaidiana na Johora ambaye hata yeye hakumbuki mara ya mwisho kutumika ni lini.

Kwa namna ligi hiyo ilivyo Diarra ana kazi ndani ya mwezi huu kabla ya kuuaga mwaka kwa michezo mitano ukiwamo wa leo wa ASFC. Mechi zijazo ni dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Azam na Mtibwa Sugar kisha kwenda Zanzibar kwa Kombe la Mapinduzi 2023 itakayofanyika kati ya Januari 1-13 mwakani itakayoshirikisha timu 12, ikiwamo Simba, Namungo, Azam na Singida Big Stars za Bara; KMKM, KVZ, Mlandege, Malinzi, Chipukizi na Jamhuri za Zanzibar na Agle Noir ya Burundi.

Chanzo: Mwanaspoti