Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Matampi kwenye vita yao ya mwisho

Diarra Matampi WA0001 Diarra, Matampi

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu zote 16 ziko viwanjani leo kuanzia saa 10:00 jioni huku asilimia kubwa zikiombeana dua mbaya.

Lakini kuna bato nne za kuvutia zinazosubiriwa kwa hamu. Bato ya kwanza ni hii ya kugombania kuwa Kipa Bora wa msimu huu ambapo hadi sasa Djigui Diarra wa Yanga na Ley Matampi wa Coastal Union ndio wanaochuana katika tuzo ya Glovu ya Dhahabu kutokana na wote kufikisha ‘Clean Sheets’ 14 katika Ligi Kuu msimu huu.

Wote ni raia wa kigeni. Diarra anaipambania tuzo hii kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuchukua misimu miwili iliyopita lakini kwa Matampi huu ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union akitokea Klabu ya Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya kwao DR Congo.

Makipa wote wawili wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu zao hadi sasa ambapo Diarra ameiwezesha Yanga kutetea taji lake la ligi huku kwa upande wa Matampi akiiwezesha Coastal Union kumaliza nafasi ya nne na kufuzu michuano ya kimataifa msimu ujao.

Vita ya Matampi na Diarra inaangaliwa zaidi ili kujua ni nani kati yao ataibuka kidedea kutokana na msimu bora waliokuwa nao. Nani anastahili Tuzo ya Kipa Bora msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live