Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Manula wapewa dili tamu

Manula Penalty Save.jpeg Manula akiokoa Penati dhidi ya Hporoya

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba itakuwa wenyeji wa Raja Casablanca ya Morocco katika Ligi ya Mabingwa, huku Yanga itaikaribisha TP Mazembe ya DR Congo katika Kombe la Shirikisho Afrika, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Pondamali aliliambia Mwanaspoti kuwa, kwa ajili ya kuhakikisha wanazibeba timu zao na kujipungizia majukumu mengi ni lazima makipa hao wazungumze na mabeki wao muda wote ili wasifanye makosa katika michezo za wikiendi hii.

Katika mechi za kwanza kwa timu hizo ugenini, Yanga ikilala 2-0 kwa Monastir ya Tunisia na Simba kufungwa 1-0 na Horoya ya Guinea, timu zote zilifungwa mabao ya aina moja ya mipira ya kutengwa (kona na faulo), kitu ambacho Pondamali alisema imetokana na makipa hao kutozungumza na mabeki na kuwashauri lazima wawe wakali kama wanataka kuzibeba timu.

Pondamali alisema makipa ni sawa na kocha wakiwa uwanjani hivyo wanatakiwa kuzungumza muda wote bila kuogopa na wasiwafanye mabeki wao kuwa marafiki na endapo wataona mabeki hawafanyi ipasavyo basi waokoe hatari hizo kabla hazijafika langoni mwao.

Alisema katika michezo ya ugenini Manula na Diarra hawakufanya makosa isipokuwa mabeki wao waliwaangusha, jambo ambalo halipaswi kutokea kwenye mitanange ya wikendi hii.

“Makipa wanatakiwa waongee masaa yote na kuongea siyo kwamba unaogopa mechi kwani kipa ni sehemu ya kocha anaelekeza, kipa rafiki yako ni nyavu tu siyo mabeki na ukiona mabeki wanafanya uzembe toka haraka pangua mpira,

“Mabeki siku zote ni wazembe kuruka ukiwategemea watakufungisha sana, mpira kule unakotoka siyo hatari ila unakoishia ndiyo hatari zaidi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Mashujaa FC ya Kigoma.

Kuhusu mechi dhidi ya TP Mazembe na Raja Casablanca, alisema silaha kubwa kwa Simba na Yanga kupata matokeo mazuri ni kujituma dakika zote 90, kutoruhusu wapinzani kucheza mpira, kupata faulo nje ya 18 na kuwataka viongozi kuhamasisha na kutoa motisha kwa mastaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live