Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Lomalis kukosa Coastal Union

Lomalisa Diarra Diarra, Lomalis kukosa Coastal Union

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa leo Jumatano wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Yanga Sc wanatarajia kuwakosa nyota wawili, Djigui Diarra na Joyce Lomalisa.

Nyota hao watawakosa kutokana na sababu mbalimbali ambapo Diarra alipata maumivu ya bega kwenye Karikakoo Dabi wakati tukiifunga Simba magoli 5-1.

Kwa upande wa Lomalisa, yeye ana matatizo ya kifamilia, hivyo hakusafiri na timu kuelekea Tanga.

Ukiachana na nyota hao, wengine waliobaki na kusafiri na timu, wapo tayari kwa mchezo huo ambapo ni muhimu kurudi Dar na pointi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live