Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Bacca, Kibabage kuwania tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi Yanga

Kibabage Bacca Diarra Diarra, Bacca, Kibabage kuwania tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi Yanga

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majina ya wachezaji watatu wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga kwa Mwezi Desemba, yamewekwa hadharani.

Wachezaji wanaowania tuzo hiyo inayotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ni Nickson Kibabage, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ na Djigui Diarra.

Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana baada ya kupigiwa kura na mashabiki kupitia application ya Yanga SC.

Tuzo hizo zimeanza kutolewa mwezi Oktoba 2023 chini ya udhamini wa NIC, ambapo mshindi alikuwa Stephane Aziz Ki, kisha Novemba tuzo ikaenda kwa Pacome Zouzoua.

Washindi wote wa tuzo hizo, kila mmoja amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni nne.

Nani atashinda tuzo hiyo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live