Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra, Aziz Ki kuwakosa Dodoma Jiji leo

Diarra, Aziz Ki Kuokosa Dodoma Jiji Leo Diarra, Aziz Ki kuwakosa Dodoma Jiji leo

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra na kiungo wao mshambuliaji Aziz Ki, hawatakuwa sehemu ya mchezo leo watakapokuwa kibaruani dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Yanga waliotoka kuangusha alama mbili mchezo uliopita baada ya kutoka sare dhidi ya Kagera Sugar, watakuwa kwenye uwanja wa Azam Complex leo Februari 5, 2024 kuwakabili Dodoma.

Akiuzungumzia mchezo huo, Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema watawakosa nyota hao ambao bado hawajarejea nchini kutoka kwenye majukumu ya timu zao za Taifa katika michuano ya Afcon.

"Tumewapa siku mbili ambazo tunaamini watakuwa wamesharejea nchini na wataungana na timu," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live