Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diarra Ampa Mbinu Mshery Yanga

Yanga 3.png Diarra Ampa Mbinu Mshery Yanga

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kutua Yanga, kipa Aboutwaleeb Mshery, amefunguka kuwa ana matumaini makubwa ya kupata nafasi katika kikosi cha kocha Nabi kwani amekuwa akijifunza vitu vingi kutoka kwa kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra kwa kipindi chote ambacho alikuwa na Mtibwa.

Amesema anaamini katika kujifunza kwa makipa wenye uwezo mkubwa na kuongeza bidii zaidi ili kumshawishi mwalimu. Yanga ilimtambulisha rasmi mchezaji huyo jana (juzi) kama kipa wao.

Mshery amethibitisha kuwa mipango yake baada ya kujiunga na familia ya Wanajangwani ni kuhakikisha anapambana ili aweze kumshawishi Nabi aweze kumpa nafasi ya kuanza lakini pia amekuwa akijifunza vitu vingi kutoka kwa makipa wakubwa kama Diarra ambaye atakwenda kuchezaAfcon akiwa na kikosi cha Mali.

“Kwanza kabisa nina furaha ya kujiunga timu kubwa kama Yanga lakini nina kazi kubwa ya kuhakikisha napambana ili niweze kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kocha Nabi.

“Diarra ni kipa mzuri na nimekuwa nikimfuatilia kwa kipindi kirefu, pia nimejifunza vitu vingi sana kupitia yeye, hivyo kucheza naye timu moja kwangu ni jambo zuri na ninaamini nitajifunza vitu vingi kupitia yeye lakini pia kikubwa nahitaji zaidi ushirikiano kutoka kwa makipa wenzangu Erick Johora na Djigui Diarra, pamoja na wachezaji wenzangu ili tufikie malengo ya Yanga ambayo ni kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mshery.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live