Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Haji Manara alipaswa kufunguliwa kifungo cha mpira

Diamond Na Manara Diamond: Haji Manara alipaswa kufunguliwa kifungo cha mpira

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki nchini Diamond Platnumz wakati akizungumza kwenye sherehe ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, na kumvisha pete mchumba wake Zaylissa, amesema kuwa hadi leo Haji hakupaswa kuwa amefungiwa.

Diamond amesema yeye ni miongoni mwa watu ambao wanamfuatilia sana Haji, lakini kwenye sekeseke lake la kufungiwa hata kama aliteleza, alipaswa awe amefunguliwa muda mrefu, kutokana na mchango wake nchini kwenye upande wa mpira wa miguu.

Mwaka 2022 kamati ya maadili ya TFF ilimfungia Manara miaka miwili kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya Sh20 milioni, kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyopigwa jijini Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live