Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Di Maria shangwe la ubingwa hadi mwilini

BAE861DB BCB8 4BB1 B490 51493BA60153.jpeg Nyota wa Argentina, Angel Di Maria

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Argentina Angel di Maria amechora tattoo ya Kombe la Dunia pajani ikiwa ni sehemu ya shangwe la kubeba ubingwa huo waliopata baada ya kuichapa Ufaransa kwa mkwaju wa penalti 4-2.

Di Maria alifunga bao kwenye mechi ya fainali dhidi ya Ufaransa akiisaidia Argentina kubeba ubingwa kwa mara ya tatu kwenye michuano kimataifa, miaka ya hivi karibuni.

Winga huyo anayekipiga Juventus alisherehekea ubingwa kwa kujichora tattoo ya Kombe la Dunia, huku juu ya mchoro huo akichorwa nyota tatu ikiashiria mataji matatu ya Kombe la Dunia ambayo Argentina imetwaa, ikiwamo 1978 na 1986.

Tattoo hiyo ilichorwa na Ezequiel Viapiano na kisha Di Maria akatupia picha hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi milioni 22.9 akiambatanisha na ujumbe mfupi na kumshukuru mchoraji wake.

“Kwenye ngozi maisha yangu yote, asante sana rafiki yangu, hakika iliandikwa (mbinguni ushindi huu) kwa ajili yetu (Argentina), twende zetu Argentina,” aliandika Di Maria.

Mashabiki wa Di Maria walimsifu wengine wakisisitiza hakika Argentina ilistahili kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia kutokana na kiwango bora walichoonyesha kwenye fainali hizo za Qatar.

Wakati huo huo, Di Maria amesisitiza hataondoka Juventus katika dirisha dogo litakapofunguliwa mwezi ujao, akisema hakuwa na mipango yoyote ya kutimka baada ya fainali za Kombe la Dunia. Awali taarifa ziliripoti Di Maria angeondoka katika dirisha dogo la usajili.

Baada ya fainali za Kombe la Dunia, Di Maria alikwea pipa hadi Argentina kusheherekea mafanikio waliyopata pamoja na wachezaji wenzake.

Chanzo: Mwanaspoti