Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dest kumuondoa Wan - Bissaka Man United

Ot Pic Data Sergino Dest

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Klabu ya Manchester United ipo katika mikakati ya kumsajili beki anayekipiga Barcelona, Sergino Dest, 21, anayepatikana kwa mkopo kukiwa na kipengele cha kununuliwa jumla.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni Sky Sport imedaiwa kwamba uhamisho huo utawezekana endao Aaron Wan-Bissaka ataondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Imeelezwa Wan –Bissaka yupo mbioni kusepa baada ya kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza kwani si chaguo namba moja wa Erik ten Hag.

Licha ya Diogo Dalot kumshawishi Ten Hag mechi mbili za Ligi Kuu England msimu huu, kocha huyo bado ameonyesha kuvutiwa na Dest.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz