Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Desemba 20 ni GSM Day

GSM (600 X 488) Ghalib Said Mohammed (GSM)

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Jumatano ya Desemba 20, 2023 ni siku ambayo Yanga SC itacheza mchezo wake wa nne wa hatua ya makundi wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana ukiwa ni mchezo muhimu kwao.

Kuelekea mchezo huo Mfadhili wa Yanga SC Ghalib Said Mohammed (GSM) amenunua tiketi zote za mzunguko za mchezo hivyo Mashabiki wa Yanga wataingia bure upande wa mzunguuko.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe ametangaza kuwa siku hiyo itakuwa ni GSM Day na Mashabiki wa Yanga siku hiyo ili kumpa heshima hiyo GSM waende uwanjani wakiwa wamevaa jezi za Yanga zenye nembo ya GSM.

GSM amekuwa chachu ya mafanikio ya Yanga kwa miaka ya hivi karibuni, hivyo Klabu hiyo imeamua kumpa heshima hiyo mdhamini wao (GSM Day) ambapo Kamwe amewataka Wananchi kufika Uwanjani wakiwa wamevalia jezi za Yanga zenye nembo ya GSM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live