Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deschamps agoma kuzungumzia mustakabali wake Ufaransa

Didier Deschamps Speka Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amegoma kuzungumza kuhusu hatima yake ndani ya kikosi hicho baada ya kulikosa Kombe la Dunia dhidi ya Argentina kwenye mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa Lusaini jijini Doha.

Ufaransa ilikuwa na matumaini ya kubeba kombe lkwa mara ya pili mfululizo lakini ikapoteza kwa Argentina kupitia mikwaju ya penalti 2-4 Emiliano Martinez akiibuka kinara baada ya kudaka penalti ya Kingsley Coman na nyingine iliyopigwa na Aurelien Tchouameni ikienda pembeni.

Deschamps, 54, aliulizwa na waandishi wa habari lakini akapotezea swali hilo akisisitiza atazungumza na shirikisho la soka Ufaransa kabla ya kufanya uamuzi.

“Hata kama tungeshinda nisingejibu hilo swali, bila shaka nina huzuni kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi, lakini hivi karibuni nitaongea na Rais wa shirikisho halafu ukweli utajulikana,” alijibu Deschamps.

Deschamps alianza kuinoa Ufaransa tangu mwaka 2012 na kuipatia mafanikio ikiwemo kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018, Russia. Vilevile kocha huyo alipata tuzo kadhaa za ukocha wa michuano mbalimbali katika historia ya soka lake.

Katika mchezo huo wa fainali Ufaransa ilijikuta nyuma kwa mabao 2-0 kabla ya Deschamps kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili kipindi cha kwanza yaliyobadilisha taswira ya mchezo, hata hivyo Ufaransa ikashindwa kwenye mikwaju ya penalti baada ya mpira kuchezwa dakika 120.

Kuhusu mabadiliko aliyoyafanya kabla ya mapumziko Deschamps aliongeza “Yalikuwa ya kimbinu, nilifanya kwasababu niliona kulikuwa na upungufu na kuna upande nguvu ilikosekana.”

Argentina iliyoongozwa na nyota wa PSG, Lione Messi iliibuka ubingwa wa Kombe la Dunia Qatar kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36 iliyopita na kutengeneza historia kwa taifa lao.

Chanzo: Mwanaspoti