Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deschamps: Mbappe hakuwa na kiwango bora dhidi ya Poland

Mbappe Deschamps Kylian Mbappe

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa Kylian Mbappe hakufanya vyema dhidi ya Poland licha ya kufunga mabao mawiliyaliyoisaidia Ufaransa kutinga hatua ya robo Fainali.

Mbappe ana mabao matano mpaka sasa katika fainali zinazoendelea nchini Qatar, huku akiwa na jumla ya mabao tisa katika michuano ya Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 23.

Licha ya ubora wake aliouonyesha, Deschamps alisema kuwa anaamini kuwa Mbappe hakuwa na matokeo yake bora kwani wanamfahamu na tayari wamemuona kwenye baadhi ya mechi.

“Hakuwa na mechi yake bora usiku wa jana, sitaki kumshtaki kwa lolote, na anajua hilo mwenyewe. Lakini anaweza kubadilisha mechi kwa muda mfupi, anacheza kwa furaha sana na anataka kushiriki naye tabasamu hizo. Ufaransa ilihitaji Kylian Mbappe mwenye ubora zaidi jana.”

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain alishirikiana na Olivier Giroud, ambaye alifungua ukurasa wa mabao dhidi ya Poland na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa lake akiwa na mabao 52, akimpita Thierry Henry ambaye alisimama tangu 2009.

Giroud alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha Ufaransa nchini Urusi katika fainali za mwaka 2018, ingawa alishindwa kufunga na sasa anajivunia mabao manne akiwa Qatar, jambo ambalo ni la kuvutia ikizingatiwa kwamba huenda angekuwa na nafasi finyu kama Karim Benzema angeendelea kuwa sawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live