Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Derby ya Dodoma, Baobab yaendeleza uteja

Fountain Gate Princes Dom Kikosi cha Fountain Gate Princess

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) Derby ya Dodoma kati ya Baobab Queens dhidi ya Fountain Gate Princess umemalizika katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa kwa Baobab kuendeleza uteja kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0.

Mabao ya Fountain yamefungwa na mfungaji bora wa Mashindano ya shule sekondari kwa Afrika, Winfrida Charles aliyefunga mawili dakika ya 32 na 42 huku bao la tatu likifungwa na Rehema Ramadhan dakika ya 89.

ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA MCHEZO HUU

Beki wa Baobab Queens Neema Charles ameweka rekodi ya kucheza dakika 1350 akianza na kumaliza michezo yote 15 ya Ligi hiyo.

Winfrida anafikirisha mabao saba msimu huu kati ya mabao 33 yaliyofungwa na Fountain Gate,kinara wa ufungaji katika klabu hiyo akiwa Cynthia Musungu mwenye mabao tisa.

Kwa matokeo haya,Fountain imefikisha alama 35 ikiendelea kubaki katika nafasi ya tatu,huku JKT Queens akiendelea kuongoza ikiwa na pointi 37 ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 36.

Katika michezo 15 iliyocheza Baobab Queens imeruhusu mabao 20 huku ikifunga 15.

Kinara wa ufungaji katika timu ya Baobab Queens ni mshambuliaji Jamila Rajabu mwenye mabao sita.

Katika michezo minne iliyokutana timu hizo Fountain Gate imeibuka na ushindi,mara tatu huku Baobab Queens mara Moja.

Msimu uliopita Boabab Queens ilipoteza michezo yote miwili kwa Fountain ikikubali kichapo cha mabao 3-1 katika mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili wakifungwa bao 1-0 katika uwanja wa Fountain Gate Arena.

Baobab ilipata ushindi katika mchezo wa Oktoba 22 mwaka jana,katika tamasha la wanawake lilofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam, waliibuka na ushindi kwa penalti 8-7 baada ya ndani ya dakika 90 timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Chanzo: Mwanaspoti