Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Derby County majanga Championship, wakatwa alama 21

Wazza Derby County yapokwa alama 21

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Derby County inayoshiriki ligi ya Championship nchini Uingereza imenyang’anywa pointi tisa zingine baada ya awali kunyang’anywa pointi 12 na kufikia pointi 21 kwa jumla walizonyang’anywa msimu huu.

Waraka uliotolewa na klabu ya Derby ni kuwa wamekubali na hawana mpango wa kukataa rufaa dhidi ya pointi 12 zilizopunguzwa mwezi septemba wala hizi 9 za sasa.

Wayne Rooney kwa sasa kichwa kinauma baada ya kukatwa jumla ya pointi 21, huku pia kukiwa na point 3 zingine za kukatwa ikiwa tu, watashindwa tena kuendana na sheria na kanuni zinazokubalika kwenye maamuzi ya klabu na ligi kwa ujumla kwenye maswala ya bajeti za fedha.

Derby County wanashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ya Championship wakiwa bado wanadaiwa pointi 3 na ikiwa imebaki michezo 29 tu, ni muda wa sala na toba ili Rooney aweze kupindua meza asishuke daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live