WINGA aliyewashika mashabiki wa Simba, Mkongo Deo Kanda amewaambia wadau wake kuwa hali yake imeimarika na hamu yake ni kuanza kucheza mechi. Siku ya mchezo wao na Yanga wa raundi wa raundi ya kwanza wa Ligi Kuu Bara ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, Kanda alitolewa nje kwa maumivu ya mguu dakika ya 46. Ulikuwa muda mchache baada ya mchezaji huyo kufunga bao la pili na la mwisho kwa Simba ambapo alicheza vizuri nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Dilunga ingawa Yanga wakasawazisha yote. Alisema: "Nilikuwa nyumbani kwa mapumziko na nimerudi Dar es Salaam kutoka Congo. Hali yangu kiafya kwa sasa niko vizuri kabisa." "Nimeanza mazoezi na hamu yangu kuanzia wiki ijayo nianze kucheza mechi za ligi kama kocha wangu (Sven Ludwig) atanipa nafasi ya kucheza,"alisema Kanda mshambuliaji anayecheza zaidi nafasi ya winga zote mbili na namba 10.