Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deo Kanda ndiyo basi tena

DEO.png Deo Kanda ndiyo basi tena

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Mtibwa Sugar iko mbioni kuachana na nyota wake mkongwe wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Deo Kanda.

Kanda aliyejiunga na klabu hiyo Desemba mwaka jana na kusaini kandarasi ya mwaka mmoja hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa, hivyo taarifa ambazo Mwanaspoti limezipata kutoka kwa viongozi nyota huyo anaachwa.

“Ni kweli tuko kwenye hatua za mwisho za kuachana naye kwa sababu mchango wake ndani ya timu ni mdogo na pia ni mchezaji wa kigeni anayelipwa mshahara mkubwa, tunahitaji kupunguza gharama,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, alisema suala la kuachana na mchezaji lipo chini ya Kocha Mkuu, Salum Mayanga kutokana na upungufu, uhitaji wa kuboresha nafasi.

“Dirisha dogo huwa kazi yake ni kuboresha upungufu ulioonekana hivyo nikiri tu ni kweli wapo baadhi ya wachezaji wataondoka na wengine wataingia kama ulivyo utaratibu wa kawaida ila hilo ni la benchi la ufundi.”

Nyota huyo alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa dirisha dogo akiwa ameshazichea timu mbalimbali za AS Vita, TP Mazembe, DC Motema Pembe, Raja Casablanca ya Morocco na Simba.

Chanzo: Mwanaspoti