Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Denmark yapiga marufuku familia Qatar

Denmark.jpeg Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Denmark

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo yamezidi kupamba moto kuelekea fainali za Kombe la Dunia. Zimbeki siku chache tu fainali hizi kuanza na tutazishuhudia timu 32 ambazo zitamenyana kuwania ubingwa wa fainali hizi Ufaransa ikiwa ndio mabingwa watetezi baada ya kulibeba mwaka 2018 katika fainali zilizofanyika Urusi.

Wakati mataifa 32 yakijiandaa kukwea pipa kwaajili ya fainali hizi wakisindikizwa na familia zao, Chama cha soka Denmark (FA) kimezuia familia za mastaa wa Timu ya Taifa Denmark wakiwemo wake na wapenzi wa mastaa hao kwenda Qatar kutoa sapoti.

Utamuduni wa Denmark ulikuwa unaruhusu wake, wapenzi na familia za wachezaji kusafiri kwa ajili ya kutoa sapoti kwa waume zao katika mashindano makubwa lakini safari hii chama hicho kimepiga marufuku.

Msemaji mkuu wa FA, Jakob Hoyer amesema uamuzi huu unazuia kuipa faida Qatar hususan kwenye masuala ya uchumi, nyota wa Manchester United, Christian Eriksen, kiungo anayekipiga Tottenham, Pierre-Emile, na Kasper Schmeichel ni miongoni mwa mastaa ambao familia zao zitabaki nyumbani baada ya kupigwa marufuku.

Mastaa wengine watakaoathirika na uamuzi huo mgumu ni beki wa Crystal Palace, Joachim Andersen, Jannik Vestergaard (Leicester City) Daniel Iversen (Leicester City) Rasmus Kristiansen (Leeds United), Christian Norgaard, Kasper Schmeichel,(Nice) Mikkel Damsgaard, (Brentford) na Mathias Jensen (Brentford).

BODI IMERIDHIA

Msemaji huyo kutoka FA, Hoyer ameliambia Gazeti la Copenhagen kwamba FA na bodi nzima imeridhia mpango huu ili kupunguza idadi kubwa ya watu watakaokwenda Qatar. “Hatutaki tuchangie ongezeko kubwa la uchumi, tumepunguza na kila kitu kwenye mstari, michuano iliyopita (Euro), wake na wapenzi wa wachezaji walisafiri na bodi nzima, lakini safari hii haitakuwa hivyo kwani tumeziuia safari hizo.”

Mbali na Denmark, Ujerumani nayo inapitia janga kama hilo kwasababu bado mwafaka haujapatikana wa wapi familia za wachezaji, wake na wapenzi wao watafikia Qatar tofauti na England.

Aidha ufumbuzi wa tatizo hili unaaminika utapatikana haraka iwezekanavyo. Ikumbukwe mastaa wa Timu ya Taifa England watasafiri sambamba na familia zao na sehemu watakayofikia ni Banana Island Resort na wataishi humu hadi fainali hizo zitakapoisha Desemba 18, mwaka huu.

Denmark iliyoko Kundi D itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Tunisia Novemba 22 kabla ya kumenyana na Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi wa fainali hizi, Ufaransa katika mchezo wa pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live