Denmark imekuwa na makubaliano na Manchester United kumpunguzia dakika za kucheza straika Rasmus Hojlund, anafichua kocha wa miamba hiyo, Kasper Hjulmand.
Hojlund ndiyo kwanza amerejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli. Nyota huyo, 21, alitolewa baada ya dakika 70 katika mchezo wa Liverpool na licha ya kwamba hakuwapo uwanjani kwa muda mrefu, Denmark imemjumuisha hivyo hivyo kwa ajili ya mechi zao za kirafiki dhidi ya Uswisi na Visiwa vya Faroe.
Katika kuelekea mechi hizo, kocha wa Denmark, Hjulmand alisema wamekubaliana na Man United kumpunguzia dakika za kucheza mshambuliaji Hojlund ili kuepuka asiumie tena kwa kuwa bado hajapona sawasawa. Kocha huyo alisema: “Tumekubaliana na Man United kuhusu muda wa kucheza kwa mshambuliaji Hojlund kwenye mechi hizo mbili. Hii kitu ni kizuri kwa upande wetu na upande wao pia.”