Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Denis Nkane kucheza kombe la Mapinduzi

Nkane Pic Data Denis Nkane

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari Mkuu wa timu ya Yanga, Youssef Mohamed amesema afya ya mshambuliaji Denis Nkane inaendelea vizuri na atashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza Januari mosi, 2023 Visiwani Zanzibar.

Akizungumza na SpotiLeo Youssef amesema mbali na kumpa matibabu pia mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kuweka mwili sawa.

“Nkane anaendelea vizuri baada ya kumfanyia vipimo na kubaini maumivu aliyoyapata hayakuwa makubwa sana, tulichofanya ni kumwanzishia tiba mapema kwa sasa anaendelea vizuri na atakuwepo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi,” amesema Mohamed.

Nkane aliumia mgongo na paja la mguu wa kulia baada ya kugongana na mchezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 Novemba 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Alishindwa kuendelea na mchezo huo na kutolewa uwanjani kwa machela na kuilazimu timu yake kucheza pungufu kwa dakika 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live