Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Denis Nkane asubiri ruhusa ya Nabi

NKANE Denis Nkane asubiri ruhusa ya Nabi

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Denis Nkane tayari amerejea mazoezini katika kikosi cha klabu hiyo, baada ya kupona majeraha ya nyonga yaliyomuweka nje tangu mwishoni mwa mwezi Desemba, mwaka jana na sasa anamsikilizia kocha mkuu, Nassredine Nabi ampe nafasi kuanza kukiwasha.

Nkane alikaa nje kwa kipindi kisichopungua wiki sita akiuguza jeraha hilo la nyonga ambalo Daktari wa Yanga, Moses Etutu alithibitisha ilivunjika mfupa mdogo na kusababisha nyonga kujikunja lakini sasa yupo fiti na tayari kwa mapambano.

Akizungumza baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa za kikosi cha kwanza cha Young Africans Nkane amesema “Niko poa sasa na siku yeyote mtaniona uwanjani nikicheza kwani nimepona tayari.”

Mbali na kiungo huyo, pia imethibitika kuwa Benard Morrison aliyekuwa nje tangu mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu akiuguza jeraha la nyonga, ameanza mazoezi mepesi, na wakati wowote ataungana na wachezaji wengine kwa mazoezi ya pamoja.

Chanzo: Dar24