Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dembele ni fundi ila ana kazi ya kufanya

Dembele PSG Dembele ni fundi ila ana kazi ya kufanya

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Kifaransa, Ousmane Dembele amekuwa na mwanzo mgumu wa maisha yake ya soka kwenye ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 baada ya kushindwa kumshawishi Luis Enrique katika wiki za mwanzoni mwa msimu.

Dembele ni miongoni mwa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, ambaye amekuwa na mikimbio ya hatari, mwenye uwezo wa kupiga vyenga pamoja na kuwa na sifa hizo za kipee bado hajaanza kuonyesha makali yake.

Fundi huyo hakuonekana kuwa na madhara dhidi ya Newcastle kwenye ligi ya mabingwa Ulaya huku akipoteza nafasi mbili za wazi hata kwenye mchezo wa ligi ya ndani Ufaransa dhidi ya Clermont Foot siku chache mapema, alishindwa kubadilika licha ya kupata nafasi nne rahisi katika sare ya 0-0.

Maamuzi ya ovyo muda mwingine yamekuwa yakimgharimu mchezaji huyo ambaye amejiunga na miamba hiyo ya soka la Ufaransa mwanzoni mwa msimu akitokea Barcelona ambako napo hakuonyesha kile ambacho kilikuwa kikitaarajiwa katika miaka yake sita kabla ya kuonyeshwa mlango wa kutokea.

Licha ya kuwa na kipaji, winga huyo anatakiwa kubadilika na kucheza kama mchezaji ajiyepevuka vinginevyo anaweza kuwa na wakati mgumu zaidi chini ya Enrique ambaye amekuwa akipenda mchezaji mwenye kujitoa.

Licha ya misukosuko yake huko Barca, kulikuwa na maana fulani kwa PSG kumnasa Dembele kwa pauni 43milioni mwezi Agosti hata hivyo kabla ya kuondoka alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Xavi.

Kwa miezi 18 alikuwa mmoja wa mawinga bora katika La Liga. Katika misimu yake miwili iliyopita Camp Nou, Dembele alifunga mabao 10 na kusaidia mengine 22. Maelewano yake na Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji ya Barca, yaliifanya timu hiyo kuwa tishio wakati wakipambana kutwaa taji la kwanza la Liga katika kipindi cha miaka mitatu.

Dembele, kwa mara ya kwanza tangu msimu wake wa kwanza kuchezea Borussia Dortmund mnamo 2016, alikuwa akifanya maamuzi sahihi. Au, angalau, alikuwa akifanya makosa mara chache. Alifunga mabao dhidi ya Atletico Madrid na Athletic Club. Alitoa pasi nzuri za mabao dhidi ya Real Valladolid na Viktoria Plzen. Huyu alikuwa mchezaji ambaye alikuwa akitimiza ahadi yake. Shida kubwa kwa winga huyo ni majeraha ambayo alikuwa akipata mara kwa mara kama unakumbuka hata Januari mwaka huu alipata tatizo la msuli wa paja. Dembele alikuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi minne na Barca ikabidi kumgeukia Raphinha badala yake.

Wakati huo, Mbrazil huyo hakuwa msaada, Barca walidondosha pointi nane. Walifunga mabao machache, kufungwa zaidi, na Lewandowski, ambaye hapo awali alikuwa kwenye kasi ya kufunga mabao 30 ya ligi, alimaliza msimu akiwa na mabao 23 pekee. Dembele hakuwa pekee aliyekosekana Pedri na Frenkie de Jong pia walikuwa nje ya uwanja kutokana na wao nao kusumbuliwa na majeraha.

Ilikuja kama sapraizi, alipoondoka kwenda PSG. Kocha wa Barcelona, Xavi alikiri, angependa kuendelea kuwa na winga huyo wa Ufaransa, lakini PSG ilikidhi kipengele chake cha kuachiliwa, na Dembele akakubali haraka kurejea katika nchi yake. Licha ya kuongezeka kwa umbo lake, Dembele pengine alihitaji mabadiliko ya mandhari. Ilikuwa, kwa nadharia, ujio mzuri wa nyumbani kwa nyota ambaye bado alihitaji kuanza upya.

Imekuwa ikidhaniwa kwa muda kuwa Dembele ni mchezaji wa kiwango cha dunia ambaye alihitaji tu nyumba sahihi ili kuwa mmoja wa mawinga bora zaidi duniani. Awali tuliongelea aina yake ya uchezaji hivyo ni kama maji ya bomba ambayo yalihitaji tu kufunguliwa sehemu nyingine.

Alionyesha uwezo wa kutosha kama kijana huko Rennes na Dortmund. Katika msimu wa 2016-17, Dembele aliigiza Ujerumani. Ingawa kulikuwa na maswali kuhusu mambo yake ya nje ya uwanja, winga huyo alidaiwa kughairi nyumba aliyokuwa akiikodisha Jurgen Klopp, alionyesha ushawishi mkubwa kwa upande wa Thomas Tuchel. Tuche alisifu uchezaji wa mchezaji huyo na kumpa kijana huyo dakika za kutosha tu kwenye kikosi chake, alikuwa mchangiaji mkuu, akifunga bao la kwanza kwenye fainali ya DFB-Pokal, na kufanya Timu Bora ya Msimu ya Bundesliga, na kushinda tuzo ya Rookie of the Season wa ligi.

Yote hayo yaliwashawishi Barca kutoa kitita cha Pauni 90 milioni ili kumsajili msimu huo wa joto huku wakitafuta mbadala wa Neymar.

Chanzo: Mwanaspoti