Mon, 29 May 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Licha ya tetesi za kuhusishwa kusepa Camp Nou, winga Osman Dembele amesema kuendelea kubaki Barcelona kwake ni furaha na lengo lake ni kuwa gwiji klabuni hapo.
Mwandishi mkongwe wa zamani kutoka Shirika la Habari la Sky Sport, Fabrizio Romano ameeleza taarifa hiyo kupitia ukurasa wa Twitter.
“Najisikia vizuri Barcelona, natamani kuwa mchezaji mkubwa sana hapa, nimeiunga mkono timu hii tangu nikiwa mdogo.”amesema Dembele.
Mfaransa huyo amewahi kuhusihwa na klabu kadhaa nchini England ikiwemo Manchester United. Mkataba wa Dembele unaisha 2024.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live