Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dembele Afanya Maamuzi Juu ya Mkataba Mpya

 109947020 Dembele Ousmane Dembele

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya muda mrefu wa mazungumzo ya mkataba kati ya Barcelona na nyota wao Ousmane Dembele, taarifa zinasema kuwa hatimaye staa huyu amefanya maamuzi juu ya hatma yake.

Mkataba wa Dembele wa sasa unaisha mwisho wa msimu huu, na klabu imepania kuhakikisha haendi kwokwote kwa sasa.

Kwa wiki kadhaa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakiendelea, Barcelona wakiwa katika nafasi mbaya ya kutoa ofa bora zaidi kutokana na hali yao ya kiuchumi kwa sasa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Footmercato, Dembele ameamua kusalia klabuni Barcelona kwa mda mrefu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa hii ni kuwa staa huyu tayari ameshazungumza na wakala wake kuwa akamilishe dili hilo ili asaini mkataba wa kusalia Barcelona hadi mwaka 2024.

Maamuzi haya ya kuongeza mkataba kwa miaka miwili yatawapa Barcelona fursa ya kutompoteza nyota waliyewekeza Euro milioni 130, ambaye anatajwa kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Xavi Hernandez.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live