Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dean Smith njia nyeupe Carrow Road.

DEAN SMITH Dean Smith

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zilikuwa ni mbio za makocha wengi lakini sasa, Dean Smith ndiye kocha pekee anayehusishwa na Norwich City. Njia ni nyeupe kuelekea Carrow Road.

Smith aliachishwa kazi na uongozi wa Aston Villa mwanzoni mwa wiki hii na nafasi yake kuchukuliwa na Steven Gerrard. Wakati Smith anaachishwa kazi, Daniel Farke naye alikua ameshapokea talaka yake kutoka Norwich City.

Bahati ya mtu usiilalie mlango wazi. Dean Smith anauwezekano mkubwa wa kurejea kwenye ukocha ndani ya EPL. Smith alikua akichuana na Frank Lampard katika kinyang’anyiro cha kutua Carrow Road. Lampard amejitoa kwenye mchakato huo na sasa, Smith amebaki peke yake!

Norwich City wataamua nani ataiongoza timu hiyo muda wowote kabla ya mchezo wao unafuata ndani ya EPL wikiendi ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live