Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dean Smith atimuliwa Aston Villa

DEAN SMITH Meneja wa Aston Villa afutwa kazi

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dean Smith amefutwa kazi katika klabu ya Aston Villa baada ya muendelezo wa matokeo mabaya ndani ya Kikosi hicho.

Uamuzi huo umekuja kufuatia kupoteza katika mechi tano mfululizo za Ligi Kuu England na mechi ya mwisho ni dhidi ya Southampton siku ya Ijumaa, aliyofungwa goli 1-0.

CEO wa Aston Villa, Christian Purslow amesema "Baada ya kuwa na mwanzo mzuri msimu uliopita, mwaka huu hatuoni muendelezo wa matokeo mazuri, kiwango cha timu na nafasi katika ligi ambapo wote ndio hasa tunapoangalia"

"Kwa sababu hiyo basi, tumeamua kufanya mabadiliko, na kuruhusu mwalimu mpya ili kuleta mabadiliko kutoka katika mwenendo tunaokwenda nao".

Dean Smith alijiunga na Villa mwaka 2018, na aliwasaidia Aston Villa kurudi Primia Ligi msimu wake wa kwanza kama Meneja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live